BALOZI SEIF AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MIILI YA WANAJESHI WA TANZANIA ( JWTZ ) WALIOUAWA DRC
Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} ikiteremshwa kwenye ndege ya JW 8029 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikitokea Mjini Dar es salaam.
Balozi Seif pamoja na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu Meja General Sharif Sheikh Othman wakitoa heshima wakati Miili ya mwashujaa ikiteremshwa kwenye ndege.
Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jassem Alnajem wa kwanza kutoka kushoto akijumuika pamoja na Viongozi wa Kiserikali katika kuipokea Miili ya askari wa Tanzania waliouawa Nchini DRC Wiki iliyopita.
Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishuhudia kuwasili kwa Miili yaWanajeshi wa Tanzania waliouawa na waasi wa ADF Nchini DRC.
Balozi Seif akiongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar katika kuipokea miili ya Makeshi ya Tanzania yaliyouawa Nchini Jamuhuri ya Kisemokrasi ya Congo.
Majeshi ya Wananchi wa Tanzania wakiichukuwa Miili ya Askari wenzao wakiwasili katika Viwanja vya Makao Makuu ya Brigedia Nyuki Migombani kwa ajili ya kuagwa rasmi Kiserikali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za pole kwenye shughuli Maalum ya Kuiaga Miili ya Wanajeshi wa JWTZ hapo Migombani Mjini Zanzibar. Balozi Seif akilaani kitendo cha wasi wa ADF Nchini DRC kuwashambulia walinzi wa amani wa JWTZ waliouwa katika Vikosi vya Umoja wa Mataifa na hatimae kusababisha vifo vyao.
Balozi Seif akiongoza baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa Kitaifa katika kutoa Heshima za mwisho kwa askari Tisa wa Jeshi la Ulinziwa Tanzania hapo Migombani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia vifo vya askari Tisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania hapo Migombani Mjini Zanzibar. Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi akiweka saini Kitabu cha maombolezo kufuatia vifo vya askari Tisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania hapo Migombani Mjini Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zubeir Ali Mulid akiweka saini Kitabu cha maombolezo kufuatia vifo vya askari Tisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania hapo Migombani Mjini Zanzibar. Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitoa Dua kwa ajili ya kuwaombea Mashuja Askari wa Tanzania waliouawa na waasi wa ADF hapo Migombani. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimfariji Mama wa Askari wa JWTZ Iddi Abdulla Ali Mama Shinuna Juma hapo Migombani.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Huzuni,
Majonzi pamoja na simanzi ilitanda ndani ya Nyuso za Wananchi wa Visiwa
vya Zanzibar wakati ndege iliyochukuwa Miili ya Askari wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) waliouawa Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC) ilipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Aman Karume.
Miili
ya Wanajeshi hao ililetwa Nchini Tanzania juzi kwa ndege Maalum ya
Umoja wa Mataifa ikitokea DRC na kupelekwa moja kwa moja Makao Makuu ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania yaliyopo Lugalo Jijini Dar es salaam kwa
ajili ya kukamilisha taratibu za kuiaga rasmi Kijeshi.
Ndege
iliyowachukuwa Mashujaa hao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya JW 8029
iliteremsha Miili ya Askari Nassor Daudi Ali, Issa Mussa Juma, Hassan
Abdulla Makame na Hamad Mzee Kamna.
Wengine
kati ya askari hao Tisa ambapo Mmoja anapelekwa Kisiwani Pemba ni Ali
Haji Ussi, Iddi Abdulla Ali, Juma Mossi Ali, Mwinchum Vuai Mohamed na
Hamadi Haji Bakari.
Akitoa
salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif alisema kuuawa kwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania {JWTZ} katika shambulio lililofanywa na Waasi wa ADF Nchini DRC
ni la Kinyama lilikiuka misingi ya Haki za Binaadamu ambalo pia ni
kinyume na makubaliano ya Ulinzi wa Amani wa Kimataifa.
Alisema Askari hao hawakutakiwa kupigwa, kupiga wala kupigana kama
walivyokuwa wakiwajibika bila ya kuwa na Silaha kubwa katika Ulinzi wa
Amani Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo { DRC}chini ya usimamizi
wa Umoja wa Mataifa {UN}.
Balozi Seif alitoa kauli hiyo wakati wa tukio Maalum la kuipokea na
kuiaga Miili ya Askari hao 9 kati ya 14 wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania {JWTZ} wakitokea Nchini DRC kupitia Dar es salaam baada ya
kushambuliwa na waasi wa ADF na kuuawa Mwishoni mwa Wiki iliyopita.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshtushwa na Taarifa za
shambulio dhidi ya askari hao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
lililosababisha Vifo na hatimae kuleta simanzi na huzuni kubwa miongoni
mwa Watanzania wote ambalo linastahiki kulaaniwa kwa nguvu zote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar,
Wazanzibari na Watanzania wote anatoa mkono wa pole kwa wafiwa wote,
ndugu, jamaa na marafiki pamoja na Wananchi wote kutokana na msiba huo
mzito kwa Taifa.
Balozi Seif alisema msiba huo ni wa Taifa zima kwa vile umemgusa kila
Raia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo jamii kwa wakati huu
inapaswa kulichukuwa tukio la vifo vya Mashujaa hao ni amri ya Mwenyezi
Muungu, hivyo hawana budi kuupokea mtihani huo.
Aliwakumbusha Wananchi hasa wale wanaoimani za Dini kurejea katika
vitabu vya Dini inavyoelekeza na kufafanua wazi kwamba kila nafsi
itaonja mauti na hivyo ndivyo wakati ulivyowakuta Mashujaa hao na tayari
wanarejea kwa Muumba wao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba kilichobakia wakati
huu ni kwa Wananchi pamoja na Ndugu na Jamaa wa Mashujaa hao
kuwasindikiza kwa kuwaombea safari na malazi mema ili Mwenyezi Muungu
awape ridhaa katika safari yao ya lazima.
Mapema Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu Meja General Sharif Sheikh Othman
akimuwakilisha Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania {CDF} Venance Mabeyo
alisema ushirikiano wa Watanzania katika kuipokea Miili ya Mashuja hao
umeleta faraja kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ}.
Meja General Sharif alisema JWTZ ni jeshi la Wanbanchi ambalo jamii
inahaki na wajibu wa kushirikiana katika shguhuli za kiulinzi na hata za
Kijamii wakati unaporuhusu.
Kamanda Sharif alisema shambulio waliofanyiwa askari wa Jeshi la
Tanzania katika ulinzi wa amani Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
kamwe haliloteteresha Jeshi la Wananchi wa Tanzani aktika ulinzi huo wa
Kimataifa.
Aliishukuru na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa jitihada
zilizochukuwa katika kuratibu maandalizi ya Miili ya Mashuja hao hadi
kuagwa rasmi Kiserikali na baadae kupelekwa kwenye makaazi yao ya kudumu
katika Vijiji walivyozaliwa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
BALOZI SEIF AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MIILI YA WANAJESHI WA TANZANIA ( JWTZ ) WALIOUAWA DRC
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
4:33 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment