Ni miaka 9, sasa tangu mwanamuziki maarufu wa mtindo wa reggae, Kutokea Afrika ya Kusini LUCKY DUBE afariki dunia.
Lucky Dube enzi za uhai wake |
Siku ya
Alhamisi ya tarehe 18 Oktoba, 2007 katika Jijini Jo’berg, Afrika ya Kusini, LUCKY DUBE alifariki, kwa kupigwa risasi. mauaji hayo yalitokea katika
kitongoji cha Rosettenville ambako wauaji wake walitaka kumpora gari
yake na hatimaye kuishia kumpiga risasi na kumuua.
Dube, alizaliwa Johannesburg Agosti 3, 1964.
Amefariki akiwa na umri wa miaka 43. Aliwahi kurekodi album karibu 20
hivi, zikiwemo Rastas Never Die, Think about the Children, Soul Taker na Trinity. Albamu yake mpya kabisa ni ile aliyoitoa 2006, ambayo aliita Respect. Dube alikuwa na mashabiki lukuki nyumbani(south africa) na duniani kote pia.
Watu wengi walipata taabu sana kumtambulisha Dube kama
Rastafarian wa “kweli”, yeye mwenyewe alipokuwa akiulizwa alikuwa
akisema, “Kama kuwa rasta maana yake ni kufuga nywele msokoto, kuvuta
bangi na kuamini kwamba Haile Sellasie ni Mungu basi mimi si Rastafarian
lakini iwapo Urastafari ni njia ya kujikomboa kisiasa, kijamii na
kimawazo basi mimi ndiye.”
Inasemekana kuwa mtu aliyechangia sana kwa Dube kupiga
muziki wa Reggae ni Peter Tosh, amabye naye aliuawa kwa kupigwa risasi
mwaka 1989. Dube anasema mirindimo ya Tosh ndiyo hasa aliyojifunza kwayo
lakini bado anakubali kuwa Bob Marley ndiye hasa mfalme wa miondoko ya
Reggae duniani. Anasema, “Isingekuwa Bob labda tusingeifahamu reggae
duniani kama tunavyoifahamu leo.”
Ni kitu cha kustaajabisha na kusikitisha kwa kuona ni
kwa namna gani mwanadamu anazidi kuwa mnyama siku baada ya siku. Sote
tutakufa siku moja lakini kifo cha Dube, ambaye alichangia kwa kiasi
fulani kufanya watu wa rangi tofauti kuweza kuishi kwa kusikilizana pale
Kusini, ni sawa na shukrani ya punda ambayo mara nyingi huwa ni mateke.
Miziki yake siku zote ilisimamia heri, wamechukua roho yake kwa shari.
Jah amlaze mahala pema peponi Ras Luck Dube.
The legendary Lucky Dube honoured on his death anniversary
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
12:38 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment