banner image

MAMIA WAMUAGA RUBANI NA MTENDAJI MKUU MSTAAFU WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI MAREHEMU KENAN MHAIKI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamriho akitoa salamu kwa niaba ya serikali wakati  wakati wa  kuaga mwili wa Rubani na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) marehemu Kenan Mhaiki Rubani  wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana  kwenda Songea mjini mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika leo Januari 4, 2017  kwenye Makaburi ya Matogoro.
Waombolezaji wakimpa mkono wa pole kaka wa marehemu Bw. Oliver Mhaiki

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu  Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kenani Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kwenda Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4 2017.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akitoa heshima zake za mwisho Picha na Robert Okanda.         
MAMIA WAMUAGA RUBANI NA MTENDAJI MKUU MSTAAFU WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI MAREHEMU KENAN MHAIKI MAMIA WAMUAGA RUBANI NA MTENDAJI MKUU MSTAAFU WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI MAREHEMU KENAN MHAIKI Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 4:49 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.