banner image

Anna Senkoro afariki dunia

Mpendwa Anna Senkoro (katikati) enzi za uhai wake  
By Herieth Makwetta, Mwananchi hmakweta@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Huenda jopo la madaktari bingwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wangeokoa maisha ya mgombea wa kwanza wa Urais mwanamke, Dk Anna Senkoro (kati katika picha) iwapo angekubali kulazwa kwa ajili ya matibabu katika kitengo hicho jana (Jumanne) usiku.

Dk Senkoro ambaye ni mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 kupitia Chama cha TPP – Maendeleo, alifariki dunia ghafla leo (Jumatano) asubuhi wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Msemaji wa Taasisi ya hiyo iliyopo Muhimbili, Maulid Kikondo amesema Dk Senkoro alifika hospitalini hapo jana saa 10.0 jioni kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo madaktari waligundua tatizo lililokuwa likimsumbua.

Kikondo amesema baada ya vipimo alishauriwa kulazwa kutokana na hali yake, lakini Dk Senkoro alikataa na kutaka kurudi nyumbani.
Anna Senkoro afariki dunia Anna Senkoro afariki dunia Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 2:50 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.