banner image

TANZIA: MDAU CHRIS LUKOSI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Kamati ya Mpito TZUK kwa masikitiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa baba mzazi wa Ndugu yetu na mwanajumuiya mwenzetu Chris Lukosi, Marehemu Mzee BONIFACE PANGAWE LUKOSI ambaye amefariki jana  tarehe 3/01/2017, nyumbani Tanzania.
Taratibu za msiba zinaendelea kufanywa na watoto wa marehemu hapa U.K. wanatazamia kusafiri kesho alfajiri kuelekea Tanzania.Tunaomba kuwaombea safari njema na Mungu awape Faraja katika kipindi hiki kigumu. Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kuwafariji watoto wa marehemu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.

Michango yote ielekezwe moja kwa moja

kwa mtoto wa marehemu Ndugu Chris Lukosi kupitia;

Account name - Chris Lukosi
Account No. 47710160
Sort Code.  60-17-31
Natwest Bank
Kamati ya Mpito TZUK Itaendelea kuwapa taarifa zaidi za msiba na mahitaji nyumbani Tanzania, Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu kuwafariji na kuwa pamoja na familia ya Marehemu 🙏🏾🙏🏾
source:https://issamichuzi.blogspot.com/
TANZIA: MDAU CHRIS LUKOSI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI TANZIA: MDAU CHRIS LUKOSI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 3:22 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.