banner image

WATOTO WATATU WAFA WAKIOGELEA BWAWANI

Watoto watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 wamekufa maji baada ya kuzama katika bwawa lililopo eneo la Ziwamboga, Mombasa wilaya ya Magharibi B, mjini Unguja.

Taarifa ya vifo hivyo imetolewa na daktari wa uchunguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Msafiri Marijani.

Daktari huyo alisema watoto hao walikufa baada ya kukosa hewa ya oksijeni baada ya kuzama katika bwawa hilo.

Miili ya watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 ilifikishwa katika hospitali kuu wa Mnazi Mmoja mjini Unguja majira ya saa sita na nusu mchana.
 

WATOTO WATATU WAFA WAKIOGELEA BWAWANI WATOTO WATATU WAFA WAKIOGELEA BWAWANI Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 11:29 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.