banner image

TANZIA: Tambwe Richard Hizza Amefariki Dunia Leo



Akithibisha Taarifa za Msiba huu,Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Ameandika Kwenye Ukurasa wake wa Instagram

"Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Kamanda Tambwe Richard Hizza, Kamanda mwingine tena amelala.

Kamanda vita vizuri umepigana, safari umemaliza, hakika umesimama imara kuipigania demokrasia, hakika Taifa litakukumbuka kwa uthubutu wako wa kuikemea Serikali katika mabaya bila woga ingawa tulikuwa kwenye kipindi ambacho kumekuwa na kuminywa kwa haki ya kutoa mawazo na kuikosoa Serikali bila hofu.

Umekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika timu ya Upinzani, tunakuahidi hatutarudi nyuma ili kukuenzi mpaka kufikia matamanio uliyoyatamani kuyaona katika Taifa letu, tunaamini safari ya kuelekea mabadiliko ya kweli bado kilomita chache tufike.
 


Wewe ni shujaa, Nakuombea kwa Mungu akupokee na upumzike kwa amani, ulisema " Nimerudi Upinzani kutubu baada ya kuona umri na siku zimekwenda, nisijekufa nipo ccm nikaishia motoni" alisema Tambwe Hizza tarehe 07/02/2018 Tandale katika kampeni za kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalim.

Kamanda Hizza amekuwa kwenye timu ya kampeni ya mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni toka siku ya ufunguzi tarehe 27/01/2018.

Upumzike kwa amani Kamanda Tambwe Hizza, Inna lillah wa inna ilayhi raji'un.

TANZIA: Tambwe Richard Hizza Amefariki Dunia Leo TANZIA: Tambwe Richard Hizza Amefariki Dunia Leo Reviewed by SHEDrack Mtawa on 1:30 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.