banner image

RATIBA RASMI YA MAZISHI YA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU (BABA KINJE)




Jumatatu tarehe 5/2/2018
- Saa 1:00 Asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
- Saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
- Saa  4:00  Asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu
- Saa 6:00 Mchana mwili kuwasili Karimjee hall kwa shughuli ya kuagwa
- Saa 6:00 Mchana  9:00 Alasiri kuaga mwili wa marehemu
- Saa 9:00 Alasiri mpaka 9:30 Alasiri msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni
- Saa 9:30  Alasiri mpaka 11:30 Jioni maziko
- Saa 11:30 Jioni 12:30 Jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa chakula cha jioni kwa waombolezaji wote
1:30 mpaka  2:45  Usiku chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 Usiku-Hitimisho la shughuli ya Mzee wetu kwa waombolezaji wote.

Tunawashukuru sana waombolezaji wote kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu. Mungu awazidishie.
Bwana ametoa, na bwana ametwaa.
Jina lake na lihimidiwe - AMINA

Imetolewa na:
Omary A. Kimbau
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi
 Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakiwasili nyumbani kwa Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru,Victoria House-Kingunge Street,Kinondoni jijini Dar jioni ya leo 
  Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh Benjamin William Mkapa akitia saini kitabu cha maombolezo,kulia kwake ni Mkewe Mama Anna Mkapa mara baada kuwasili nyumbani kwa Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru,Victoria House-Kingunge Street,Kinondoni jijini Dar jioni ya leo 
 Baadhi ya Familia,Ndugu,Jamaa na marafiki wakishusha sanduku lenye mwili wa Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru,mara baada ya kuwasili jioni ya leo nyumbani kwake Victoria House-Kingunge Street,Kinondoni jijini Dar
Mtoto wa Marehemu, Kinje Ngombale Mwiru akitoa maelekezo mafupi kwa ndugu jamaa na marafiki mara baada ya mwili wa Baba yake kuwasili nyumbani kwa marehemu jioni ya leo Victoria, Kinondoni jijini Dar es salaam. Picha na Michuzi Jr.
RATIBA RASMI YA MAZISHI YA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU (BABA KINJE) RATIBA RASMI YA MAZISHI YA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU (BABA KINJE) Reviewed by SHEDrack Mtawa on 10:10 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.