banner image

MAADHIMISHO YA 19 YA KUMBIKIZI YA PROF. HUBERT KAIRUKI



Marehemu Prof. Hubert Clemence Mwombeki Kairuki na mkewe Mama Kushubila Kairuki;  mwanzilishi mwenza wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN)
Utangulizi: 
Hospital ya Kairuki (KH), Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kwa pamoja vitashiriki katika maadhimisho ya 19 ya kumbukizi ya Marehemu Prof. Hubert Clemence Mwombeki Kairuki, muasisi wa taasisi mama inayosimamia taasisi hizo yaani Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN). 



Kumbukizi hiyo itafanyika kwa juma moja kuanzia tarehe 1 Februari 2018 na kufika kilele chake tarehe 6 Februari 2018, kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama ifuatavyo: 

* Kuweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida Bunju. 
 *Kuanzisha kliniki ya mama, baba na mtoto. 
 *Kutoa huduma za afya bila malipo kwa wananchi. 
 *Uchangiaji Damu/Blood Donation.
 *Mhadhara wa Tisa wa Kitaaluma wa kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki. 
 *Mashindano ya kitaaluma baina ya wanafunzi wa HKMU na KSN. 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Herbert Kairuki Memorial, Prof. Chales Mgone akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano nao uliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4 2018. Kushoto ni Makamu Mkuu wa HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi na Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Asser Mchomvu. 

Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Asser Mchomvu, akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4 2018. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Herbert Kairuki Memorial, Prof. Charles Mgone na Makamu Mkuu wa HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi. Picha na Robert Okanda

MAADHIMISHO YA 19 YA KUMBIKIZI YA PROF. HUBERT KAIRUKI MAADHIMISHO YA 19 YA KUMBIKIZI YA PROF. HUBERT KAIRUKI Reviewed by SHEDrack Mtawa on 10:16 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.