banner image

MWALIMU AFARIKI KWA KUKOSA PESA YA KUNUNUA DAWA YA MAFUA

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Heather Holland, 38, ambaye alikuwa mwalimu amefariki dunia baada ya kushindwa kununua dawa ya mafua kutokana na gharama yake kuwa kubwa nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mume wa marehemu Frank Holland, mkewe alipokwenda hospitali alikuta dawa hizo za mafua ni Dola za Marekani 116 ambayo ni sawa na Tshs 278, 000 hivyo akaamua kuacha kununua jambo lililosababisha kifo chake.

Frank amesema alikwenda kununua dawa hizo siku moja kabla ya kifo cha mkewe ili aanze kuzitumia lakini alikuwa amekwisha chelewa.

Heather ambaye alikuwa mwalimu wa Ikard Elementary School huko Weatherford, Texas ameacha mume na watoto wawili, wa kike mwenye miaka 10 na mwingine wa kiume mwenye miaka 7.

source:malunde
MWALIMU AFARIKI KWA KUKOSA PESA YA KUNUNUA DAWA YA MAFUA MWALIMU AFARIKI KWA KUKOSA PESA YA KUNUNUA DAWA YA MAFUA Reviewed by SHEDrack Mtawa on 4:50 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.