banner image

KWAHERI SUSANE GALINOMA KISEGA

Name: Susane Galinoma Kisega
Born:17 Mei 1966
Dead: 4 November 2017

SUSANE GALINOMA KISEGA
Mwili wa mpendwa wetu SUSANE ukiingizwa kanisani kwaajili ya ibada
Ibada ya mwisho ya mpendwa wetu Susane
Waombolezaji wakiwa kanisani


Ndugu na Jamaa wakitoa Heshima ya mwisho kwa mpendwa wetu



Mwili wa Ndugu yetu Susane ukipakiwa kwenye Gari maalum

Mume wa mpendwa Susane(aliyeketi kwenye kiti cha kusukuma)
Add caption

Mwili wa Ndugu yetu Susane Galinoma ukiwasili nyumbani kwake tayari kwa safari ya kuelekea Iringa kwa taratibu za mazishi


HISTORIA FUPI YA MPENDWA WETU SUSANE
Susane Galinoma Kisega alizaliwa tarehe 17 Mei, 1966 katika Hospitali ya Ocean Road Dar es salaam. Akiwa mtoto tisa (9) kuzaliwa kwenye familia ya marehemu Stephen Jones Galinoma na Marehemu Thobietha Mgasi Gakinoma.

1971: Alipata elimu ya chekechea katika shule ya welfare huko mkoani Mwanza ambako ndio yalikuwa makazi ya wazazi wake kwa wakati huo

1975-1981: Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Olimpio,muhimbili na Forodhani.
1982-1985: Alipata elimu ya sekondali katika shule ya Mzizima.
baada ya hapo alichaguliwa kujiunga na Chuo cha Uhazili Tabora na kupata cheti.

Alijiunga kwa mujibu wa sheria JKT kambi ya Oljoro na mlalakuwa.

MAISHA YAKE KIKAZI

  • Alifanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania
  • pia alifanya kazi katika kampuni ya Lion's Insuarance na
  • mwishoni  alifanya kazi Uniliver
Baada ya hapo alijikita zaidi katika Ujasiriamali na kuhudhuria kozi kadhaa kama kusindika na kuoka mikate hadi alipokutana na umauti wake.

NDOAAlifunga ndoa takatifu na Bw. Joseph Kisega mwaka 2000 na amekuwa katika ndoa hiyo mpaka alipopatwa na umauti.
Convida inatoa pole kwa ndugu na jamaa kwa kuondokewa na mpendwa wetu Susane Galinoma Kisega BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA.
Baadhi ya Classmate wa Ndugu Susane (aliosoma nao Mzizima)

KWAHERI SUSANE GALINOMA KISEGA KWAHERI SUSANE GALINOMA KISEGA Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 6:24 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.