banner image

Mzazi mwenza wa Zari The Boss Lady amefariki dunia

IVAN SEMWANGA ENZI ZA UHAI WAKE
 Siku chache baada ya kuwepo taarifa za kuugua ghafla kwa Ivan Semwanga a.k.a Ivan the Don, mfanyabiashara maarufu nchini Uganda na mzazi mwenza wa mrembo Zari The Boss Lady, leo May 25, 2017 imeelezwa kuwa tajiri huyo kijana amefariki dunia.katika Hospitali ya Steve Biko Academic jijini Pretoria, nchini Afrika Kusini
Taarifa za awali zilieleza kuwa mfanyabishara huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.
ZARI  NA IVAN PINDI WALIPOKUWA WAPENZI
Zari aliyezaa watoto watatu na mwanamume huyo amethibitisha kifo chake kwa kuandika katika mtandao wa Instagram akimtakia pumziko la milele.
“Mungu huwaita kwake walio wema ndiyo maana amekuchukua. Umegusa maisha na kusaidia wengi. Nakumbuka ulikuwa ukiniambia maisha mafupi acha ufurahie, sasa naelewa ulichokuwa ukimaanisha… utakumbukwa daima,” anaandika Zari ambaye alitengana na mzazi mwenzake huyo kabla ya kuwa na mahusiano na staa wa muziki hapa nchini, Diamond Platnumz aliye zaanaye watoto wawili.
Anakumbukwa kwa staili yake ya maisha ya kuonyesha fedha katika mitandao ya kijamii na kuzigawa kwa watu wenye mahitaji mara kwa mara.
Kupitia Instagram account ya Zari ameandika

Mzazi mwenza wa Zari The Boss Lady amefariki dunia  Mzazi mwenza wa Zari The Boss Lady amefariki dunia Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 7:30 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.