Born: March 10, 1957, Riyadh, Saudi Arabia
Died: May 2, 2011, Abbottabad, Pakistan
Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden alizaliwa Riyadh huko Saud Arabia katika famila ya ndugu
Mohammed bin Awad bin Laden ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana kwa nyakati hizo utajiri ambao
aliupata kwa kazi yake ya ukandarasi, Osama bin Laden alizaliwa 10,march, 1957 kwa Hamida al-Attas
alikuwa mke wa kumi katika orodha ya wake za baba yake Mohammed na ambaye alimpa taraka muda
mfupi baada ya Osama kuzaliwa, Hivyo watoto aliozaliwa tumbo moja na Osama walikuwa jumla yao
wanne akiwepo mwanamke mmoja ambaye ni dada yao.
ELIMU
Osama amehudhuria shule Al-Thager model school, na baadaye akahudhuria masomo ya Uchumi na
biashara katika chuo cha KING ABDULAZIZ. Lakini pia alikuwa na shahada ya ufundi na ya maendeleo
ya jamii. Ukweli ni kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa ni mtu mwenye bidii katika kila jambo au kazi, pamoja
na hayo yote Osama aliipenda sana dini yake kupindukia kama walivyo waarabu wengine wenye itikadi
kali, muda mwingi aliutumia kuichambua quran na kazi za kujitolea.
Osama alipendelea pia kuandika
hadithi mbalimbali, kusoma vitabu vya baadhi ya waandishi kama FIELD MARSHAL BERNAD MONTGOMERY
na CHARLES DE GAULLE, na akawa vilevile mpenzi wa mpira wa miguu ambapo alicheza fowadi ya katika
kati na timu aliyokuwa mshabiki ni ARSENAL FC
MAISHA BINAFSI
Mnamo mwaka 1974 akiwa na umri wa miaka 17 Osama aliingia kwenye maisha ya ndoa rasmi ambapo ali
mwoa Najwa Ghanem huko Latakia Siria ambaye walikuja kutengana kabla ya sept 11, 2001. Baadhi ya wa
ke zake walijulikana ni Khadijah Sharif aliyemuoa 1983 na akampa talaka 1990, Khairian Sabar aliyemuoa
1985, Siham Sar aliyemuoa 1987 na Amal al-Sadah aliyemuoa 2000, inasadikika kuwa ni baba wa watoto
kati ya 20 mpaka 26 kwa wake zake wote. Watoto wake wengi walikimbilia Iran baada ya mashambulizi ya
baba yao ya sept 11 na 2010.
mamlaka husika huko Iran zinataja kuwa bado zinaendelea kudhibiti mien
endo yao. Mwanae mmoja wa kiume na ambaye alikuwa ni bodyguard wake anaeleza kuwa baba yake ali
kuwa ni mtu mtafiti sana mkali kupindukia japo aliipenda sana familia yake na alikuwa na kawaida ya
kuitoa familia yake nje kutalii na kustarehe kwenye fukwe mbalimbalil
Baba yake Osama bin Laden alifariki 1967 kwa ajali ya ndege Saud Arabia, pia kaka yake Salem
bin laden aliuawawa San Antonio huko Texas USA
IMANI YAKE
Osama bin Laden alikuwa akiaminia kuwa marekani wanawachukia sana waislam sio kwa sababu ya jinsi
walivyo bali kwa sababu ya yale wanayotenda, pia akaongeza kuwa ni sheria ya SHARIA pekee ndiyo ita
kayowaweka huru toka kwenye unyanyasaji wa marekani kwenye ulimwengu wa kiislam, na bado aliamini
kuwa Afganistan chini ya utawala wa Mullah Omars Taliban ndiyo nchi pekee ya kiislam Duniani, bado
alikuwa na mpango wa kuiangamiza Israel na kuilazimisha marekani kuiachia mashariki ya kati
MAISHA YAKE JESHINI
Baada ya kuhitimu elimu yake ya chuo, Osama alikwenda pakistani ambako alitumia fedha na mali zake za
urithi katika kumsaidia Abdullah Azzam ambaye alikuwa na jeshi lililokuwa likipinga vita ya kisoviet huko
Afganistan
|
No comments:
Post a Comment