Yapata miaka minne(4) sasa,tangu msanii maarufu na nguli nchini Tanzania Bara na Visiwani, Fatuma binti Baraka au maarufu kwa jina la Bi. Kidude Afariki dunia
Msanii maarufu na nguli nchini Tanzania Bara na Visiwani, Fatuma binti Baraka au maarufu kwa jina la Bi. Kidude |
Born: 1910, Zanzibar, Tanzania
Died: April 17, 2013, Zanzibar City, Tanzania
Style: Taarab
Genre: World
Awards: WOMEX, Orders, decorations, and medals of Tanzania
Albums: Zanzibara, Vol. 4: The Diva of Zanzibari music, Zanzibar, Bi Kidude with Sahib El Arry
|
Inasadikiwa kwamba mnamo mwaka 1920 tayari nguli huyu wa taarab alikuwa ameanza kuimba katika vikundi vya sanaa kwao. Taarifa zinasema mwaka 1930 Bi. Kidude alijiunga na Egyptian Musical Club ya jijini Dar es Salaam kabla ya kuliacha kundi hilo mwaka 1940 na kurejea Zanzibar.
Hakuna anayepinga kutokana na historia yake, Bi Kidude ni miongoni mwa magwiji wa muziki katika Bara la Afrika. Hakuna anayejua tarahe rasmi ya kuzaliwa nguli huyu wa muziki hadi sasa, japokuwa inakadiriwa kuwa ana umri wa miaka 102.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Bi. Kidude aliwahi kuzitoa, anaeleza kuwa alianza fani hiyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 10 na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi. Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi. Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.
Taarifa zinaeleza alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling’ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji.
Bi Kidude Enzi za uhai wake akifanya onyesho |
Watu wanasema ‘Utu uzima dawa’ Bi. Kidude alikuwa na upeo mkubwa wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na kuvaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu.
Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar. Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.
Muziki aliyokuwa akiimba ni Bi. Kidude ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrika umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.
Bi. Kidude amewahi kushinda na kutunukiwa tuzo mbalimbali: mwaka 2005 alishinda tuzo ya ‘WOMEX’ ikiwa ni kutambua mchango wa mwanamuziki huyo katika tasnia ya muziki na tamaduni za Zanzibar. Amekwisha pata tuzo tena ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha.
Rais Jakaya Kikwete pia alimtunuku Bi. Kidude Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mchango wake katika sanaa nchini mwaka 2012. Bi. Kidude. Baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa jang’ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.
Yapata miaka minne(4) sasa,tangu msanii maarufu na nguli nchini Tanzania Bara na Visiwani, Fatuma binti Baraka au maarufu kwa jina la Bi. Kidude Afariki dunia
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
10:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment