Msanii Kalanga akiwa na Elias Mnyamwezi
Msanii wa nyimbo za asili maarufu kwa jina la Kalanga "Ng'wana Kolagwa" amefariki dunia jana Jumatano Februari 21,2018 majira ya saa 11 alfajiri.
Kalanga amefariki dunia nyumbani kwao katika kijiji cha Chambo - Mwamakumbi Nzega mkoani Tabora kutokana na kile kinachoelezwa kuwa alikuwa anaumwa kwa muda mrefu.
Mazishi yanatarajia kufanyika kesho Alhamis Februari 22,2018 saa nane mchana nyumbani kwao.
Convida Funeral company inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki bila kuwasahau mashabiki wa marehemu na wapenzi wote wa nyimbo za asili kutokana na msiba huu.
Mungu ailaze Mahali pema peponi roho ya marehemu Kalanga amina!
ANGALIA HAPA BAADHI YA NYIMBO ZA KALANGA
Tanzia : MSANII WA NYIMBO ZA ASILI KALANGA AFARIKI DUNIA
Reviewed by SHEDrack Mtawa
on
8:32 AM
Rating:

No comments:
Post a Comment