|
Huyu ndo Mwamba Kapera enzi zake.... |
Kufuatia kifo cha beki wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa
Stars” Omary Kapera (wa tatu toka kulia) ,Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa
ya kifo cha beki huyo wa zamani. Rais Karia akitoa salamu za rambirambi
amesema ni masikitiko makubwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wa zamani
aliyeitumikia pia timu ya taifa. "Nimeshtushwa na taarifa hizo za kifo
cha Kapera hasa ikichukuliwa bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza
mchezaji mwingine wa zamani Athuman Juma Chama,kwa niaba ya Shirikisho
natoa pole kwa wote walioguswa na msiba huo kuanzia kwa
familia,ndugu,jamaa na marafiki.”Alisema Rais Karia. Wakati wa uhai wake
akicheza mpira amecheza katika klabu za Pan Africans na Yanga huku
akipata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania
“Taifa Stars” Kufuatia msiba huo TFF itatoa rambirambi kwa familia ya
Kapera.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF
Convida Funeral Home Company Ltd Imepokea Kwamasikitiko Makubwa taarifa ya msiba wa mpendwa wetu Omary Kapera.
Tunatoa pole kwa Familia, ndugu, jamaa, Marafiki, Na Wadau wote wa Soka Tanzania kwa Msiba huu Mkubwa Uliotupata kuondokewa na Mpendwa wetu Omary Kapera. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
No comments:
Post a Comment