Mpendwa Ndugu Dominic Mtazama Gama |
ELIMU NA KAZIMarehemu Dominic Mtazama Gama alisoma Elimu ya Msingi na Sekondari Tanzania na Uganda na kuhitimu vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa nyakati mbalimbali alihudhuria Course mbalimbali na kujiunga na jeshi la kujenga Taifa Mgulani. Baadae aliajiriwa na jeshi la polisi na baada ya muda mfupi alihamishiwa ofisi ya Rais mpaka alivyostaafu mwaka 1978 RTC Ruvuma kama mwakilishi wa mauzo, (Sales Representative Dar es Salaam).
Baadae alianzisha gazeti la hoja akiwa Mwenyekiti wa gazeti hilo na aliendelea kuwa Mwenyekiti hadi umauti ulivyomfika.
Katika Maisha yake marehemu aliwahi kuwwa kiongozi wa timu ya majimaji na Mjumbe wa FAT Taifa (sasa TFF)
Alikuwa mfadhili mkubwa wa makanisa ya kikatoliki Mwananyamala na Marungu Tanga.
Alikuwa mfadhili wa kwaya katika Makanisa yote hayo mawili Mwananyamili na marungu Tanga.
Marehemu alikuwa mlezi wa karibu wa familia zote kina Gama,Lugusha,Nyoni na Watu mbalimbali Dar es salaamu, Tanga, Songea na Marungu kwa Mapendo makubwa sana.
KUOA Marehemu alifunga ndoa ya Kikatoliki tarehe 29/11/1980 katika kanisa Katoliki Mwananyamala na Bi Nyaso Lugusha Gama, alibahatika kupata watoto (5) kati yao wawili wametangulia mbele ya haki nao ni William dominic na Joseph Dominic Gama, Marehemu ameacha mjane na watoto watatu (3).
UGONJWATarehe 13/08/2017 aliugua kiarusi kutokana na shinikizo la damu hadi kupelekwa kulazwa Hospitali ya Mzena, baadae alihamishiwa Muhimbili mpaka pale familia ilipoamua kumpeleka Afrika kusini kwa matibabu zaidi ambapo iligundulika kwamba mishipaya kichwa imejaa mafuta (cholesteral) tarehe 20/11/2017.
Tokea afanyiwe upasuaji huo hali yake haikuweza kuimarika vizuri hadi umauti ulipomkuta tarehe 28/11/2017 katika Hospital ya MEDICLINIC MIDSTREAM PRETORIA nchini Africa kusini.
SHUKRANI
- Shukrani za dhati ziwaendee Madaktari, Wauguzi, Wafanyakazi wote wa Mzena Emilo, Muhimbili na Mediclinic Midstream Pretoria nchini Afrika kusini, Askofu wa jimbo la Katolic Tanga na Parokia ya Kanisa la Katoliki Mwananyamala.
- Shukrani maalum ziwaendee 1. Mej. Gen. Semfuko, kwa Upendo wa hali na mali. 2. Familia ya Mulla wa Dar es salaam na Pretoria Afrika Kusini na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Mwisho tunawashukuru wana Jumuiya wote wa marangu na Dar es Salaam majirani, ndugu na marafiki walioungana nasi kufanikisha mazishi ya ndugu yetu mpendwa Dominic D. Gama kwa hali na mali.
"RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE"
Mamia ya waombolezaji walijitokeza kutoa heshima za mwisho kwa Mpendwa Baba yetu Dominic Mtazama Gama (nyumbani kwake Kinondoni Dar es Salaam) |
Dada Vick Lugongo akitoa heshima ya mwisho nyumbani kwa Marehemu Dominic Gama |
Waombolezaji wakisikiliza wimbo wa kwaya ya Kanisa Katoliki Mt. Martin Mwananyamala Dar es salaam
Maryam Gama (mtoto wa Marehemu) akiwa na Deborah Nyoni , Mara baada ya kuweka shada la Maua katika kaburi |
(kutoka kushoto) Vick Haule, Maryam Gama, Deborah Nyoni,pamoja na Mama Siwa wa Songea baada ya kuweka Mashada ya maua katika Kaburi la mpendwa wetu Baba Dominic Gama
(kutokea kushoto)Tatu Gama, Martha Gama, Mrs Alice Mkanula, Maryam Gama, Deborah Nyoni, Mama Gama wa Songea Mara baada ya kuweka mashada la Maua katika kaburi la Mpendwa Baba Dominic Gama
(kutokea kushoto) Mariam Gama, Debora Nyoni, Mke wa Marehemu Nyasu Ganma pamoja na ndugu Valance Matunda
Convida Funeral Home Company Ltd Inatoa pole kwa Ndugu, Familia, Marafiki, Jirani na wote kwa Msiba huu Mkubwa wa kuondokewa na Mpendwa Baba yetu Dominic Mtazama Gama. Twamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi Amina
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake liimidiwe
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake liimidiwe
UTAKUMBUKWA DAIMA MPENDWA WETU BABA DOMINIC MTAZAMA GAMA (11.11.1948 - 28.11.2017)
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
7:38 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment