Ndugu Bendera aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Stars pekee iliyoshiriki fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 1980 kule Nigeria, amekumbwa na
mauti hayo masaa manne tu tangu alipofikishwa Muhimbili akitokea mjini
Bagamoyo. KOCHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Joel Nkaya Bendera, amefariki dunia jana Jioni (jumatano) katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam. Bendera aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Stars pekee iliyoshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 1980 kule Nigeria, amekumbwa na mauti hayo masaa manne tu tangu alipofikishwa Muhimbili akitokea mjini Bagamoyo. Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha kifo cha mwanamichezo huyo maarufu, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge (Korogwe Mjini), Naibu Waziri wa Michezo, Habari na Utamaduni. Pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa (Morogoro kisha Manyara). "Ni kweli Joel Bendera amefariki. Aliletwa leo saa 6:30 kwa gari la wagonjwa akitokea Hospitali ya Bagamoyo, ilipofika saa 10:24 jioni alifariki,” amesema Aligaesha. Mwanaspoti ilipotaka kujua chanzo cha kifo chake, alisema: “Hilo ni suala la familia, lakini kwa wakati huu itoshe kusema amefariki.” Katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli Oktoba 26, Bendera alikuwa miongoni mwa wakuu wa mikoa waliostaafu na nafasi yake imechukuliwa na Alexander Mnyeti aliyepandishwa kutoka Mkuu wa Wilaya ya Arumeru. Convida inatoa pole kwa ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu wa mpendwa wetu Joel Bendera, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake liimidiwe. Amen |
TANZIA: Mh. Joel Bendera afariki dunia
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
10:30 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment