SharoMilionea |
Msanii Ali Kiba, Producer C9 na Sharomilionea enzi za uhai wake |
Msanii huyo ambaye mashabiki wake wengi walikuwa ni vijana na watoto pamoja na wazee, alikuwa akibuni staili mbalimbali kuvutia mashabiki wake hususa kwa kutia madoido ya Kimagharibi na kujiweka katika maisha ya juu katika uigizaji wake.
Baadhi ya Nukuu za Sharomilionea alipokuwa akihojiwa na waandishi..kwenye redio na tv
“..Niliamua kuwa mbunifu ili kutafuta staili tofauti na wachekeshaji wengine na ninashukuru hilo limeweza kufanikiwa," alisema mchekeshaji huyo."
Sharomilionea (Enzi za uhai wake) akiwa na Majuto |
"Niko tofauti sana na vile jamii inavyoniona kupitia maigizo yangu...huwa sipendi kuishi maisha kama yale ila pale nipo kazini ndio maana ninaonekana vile," alisema.
Alisema lengo lake la kuigiza staili ya aina ile ni kuwafundisha wenye tabia kama hizo kuacha kwani binadamu wote ni sawa na hakuna aliyebora kuliko mwingine.Hussein Ramadhani "...kuna baadhi ya watu katika jamii wanapokuwa na maisha tofauti na watu wengine hupenda kujionyesha na kuwadharau wenzao ambao maisha yao ni yakawaida na kwamba jambo hilohalipendi katika maisha yake.
“Binafsi siishi maisha yale na wala siyapendi kabisa maana nawaonyesha ili waweze kuachana na tabia hizo kwa kuwa hazina maana yoyote zaidi ya kuonyesha ni jinsi gani walivyokuwa malimbukeni kuiga maisha ya watu wa Magharibi”anasema.
Kwa mujibu wa Mchekeshaji huyo, alikiri kwamba asingeweza kufikia alipofika bila ya Mzee Majuto ambaye alimfundisha mambo mengi ya sanaa.
Alisema Mzee Majuto alimsaidia kwa kiasi kikubwa kufikia hapo alipo na kamwe hawezi kusahau mchango wake katika tathinia ya sanaa hapa nchini.
"Ninawashukuru wasanii wenzangu wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamenipa msaada mkubwa hadi kufikia hapa nilipo...Mzee Majuto ni jembe langu ambalo siwezi kulisahau katika maisha yangu yote ," alisema.Hussein Ramadhani licha ya kujikita katika sanaa ya vichekesho lakini anajihusisha na muziki wa kizazi kipya ambapo pia ameonyesha kiwango cha hali ya juu kutokana na staili ya uimbaji wake.
Miongoni mwa nyimbo alizoziachia hewani msanii huyo ni pamoja na Sondela na Hawataki alioshirikiana na Rich Mavoko pamoja na Kanali Top zilifanikiwa kumuweka katika nafasi nzuri katika chati za muziki.
Muigizaji Kitale Teja na Sharo milionea enzi za uhai wake |
Historia ya mchekeshaji huyo, inaonyesha alianza kujikita katika sanaa tangu akiwa shule ya msingi Tanga na alipomaliza alifanikiwa kuja Dar es Salaam na hapo kipaji chake kilizidi kukua na kujipatia umaarufu baada ya kukutana na muigizaji mkongwe Mzee Majuto na kujiingiza moja kwa moja katika Vituko Show.
Baadhi ya filamu alizoshiriki mchekeshaji huyo kwa kushirikiana na Mzee Majuto na wasanii wengine ni pamoja na Chuma Ulete, Pedeshee, Vyumba vimejaa na Kozi Man.
MIAKA MITANO (5) YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MSANII SHAROMILIONEA
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
2:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment