banner image

Tanzia:Mwanamziki mkongwe Shabani Dede afariki Dunia.

SHAABAN DEDE
MWIMBAJI mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa. Dede, mwanamuziki wa Msondo ambaye pia aling’ara na bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee na OSS, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari pamoja na figo.
Hamad Dede, mtoto wa marehemu, amesema kwamba mpendwa wao huyo amewatoka. “Baada ya kama masaa mawili tutakaa kama familia na kutoa taarifa rasmi ya msiba utakuwa wapi na mazishi ni lini ingawa kuna kuna zaidi ya asilimia 70 kuwa tutazika kesho,” alisema Hamad.
Onyesho la mwisho Dede kushiriki ni lile lililofanyika Travertine Hotel, Magomeni la mpambano wa Msondo na Sikinde Mei 20 mwaka huu.
HISTORIA YA NDUGU SHABAAN DEDE
Shabani Dede maarufu kama Super Motisha, alianza kuwika kwenye tasnia ya muziki wa dansi akiwa kwenye bendi ya Dodoma International. Naweza kusema uwezo katika utunzi na uimbaji wake uliwashawishi viongozi wa Msondo Ngoma ambayo kwa wakati huo ilikuwa inaitwa Juwata Jazz wamuite kwenye bendi hiyo mwaka 1980 miaka michache tu baada ya kipaji chake kuonekana akiwa kwenye bendi ya Dodoma.
Sababu kubwa iliyowashawishi viongozi wa Msondo Ngoma ni uwezo wake wa kufanana na kuweza kuziba pengo la Hassani Bitchuka, ambaye alinyakuliwa na watani wao wa jadi, DDC Mlimani Park au Sikinde Ngoma Ya Ukae.
Akiwa ndani ya Msondo Ngoma alifanikiwa kuandika nyimbo lukuki zilizopata nafasi ya kuvuma na kupendwa na mashabiki wa bendi hiyo, miongoni mwa ngoma hizo ni wimbo unaoitwa Jane, Christopher, Fatuma Maisha ni Vita na nyingine nyingi.
Mahasimu wa Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae walifanikiwa kumchukua na kumhamishia kwenye bendi yao ambako akiwa ndani ya Sikinde, mkono wake ulitumika kuandika nyimbo kama vile Talaka rejea na Diana.
Mahasimu wa Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae walifanikiwa kumchukua na kumhamishia kwenye bendi yao ambako akiwa ndani ya Sikinde, mkono wake ulitumika kuandika nyimbo kama vile Talaka rejea na Diana.
Hakudumu kwenye bendi hiyo kwani mwaka 1984 aliipa kisogo Sikinde na kuhamia Bima Lee Magneti Tingish huku akiwa kinara kwa kutunga na kuimba nyimbo kama Dunia duara, Shangwe ya Harusi, Zenaba, Aziza pamoja na Nusu Kilo.
Inaaminiwa kuwa msanii kutoka bendi moja kwenda nyingine ni kukua kisanaa hivyo Shabani Dede, alihamia Orchestra Safari Sound (OSS) ambapo ndani ya bendi hiyo alifanya vyema na nyimbo kama vile Nyumba ya Mgumba na warithi ambazo ziliipandisha chati bendi hiyo na kufanya azidi kufahamika zaidi. Nyumbani ni nyumbani ndivyo wahenga wanavyosema, haikuchukua muda mrefu ndani ya Orchestra Safari Sound (OSS) alirudi nyumbani kwake Msondo Ngoma ambako yupo Hadi alipofikwa na umauti.
Tanzia:Mwanamziki mkongwe Shabani Dede afariki Dunia. Tanzia:Mwanamziki mkongwe Shabani Dede afariki Dunia. Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 6:30 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.