banner image

TANZIA : KIFO CHA SETH KATENDE (Bikira wa Kisukuma)

SETH KATENDE ENZI ZA UHAI WAKE
Kwa majonzi makubwa, uongozi na wafanyakazi wote wa Efm radio na tv-E , unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende – maarufu kama bikira wa kisukuma kilichotokea Julai 9 katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Ni vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwakuwa sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba mwenyezi mungu aipumzishe roho ya mpendwa wetu seth katende mahali pema, Amina.
Uongozi na wafanyakazi wa Efm radio na tv-E unatoa pole kwa familia ya ndugu yetu seth na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.
Seth Katende (Bikira wa Kisukuma) enzi za uhai wake akiwa  studio, Efm redio
Kutoka kushoto mpendwa Seth Katende akiwa na timu nzima ya kipindi cha ubaoni alichokua akitangaza.

CONVIDA FUNERAL HOME Tunatoa pole kwa Familia ,wafanyakazi wa efm na wote kwenye kipindi hiki kigumu cha kumpoteza Mpendwa wetu Seth katende, Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake liimidiwe... Amen
TANZIA : KIFO CHA SETH KATENDE (Bikira wa Kisukuma) TANZIA : KIFO CHA SETH KATENDE (Bikira wa Kisukuma) Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 11:14 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.