banner image

Tanzia: MKE WA MZEE YUSUF 'BI CHIKU' AMEFARIKI DUNIA

 Mke mdogo wa Mwimbaji wa zamani wa Jahazi Modern Taarabu Alhaj Mzee Yusuph Chiku amefariki usiku wakuamkia leo wakati anajifungua na mtoto naye amefariki.
Kupitia Instagram yake Mtangazaji wa Clouds FM Geah Habib ameandika: >>>”Innalillah wainaillah rajuun mke mdogo wa Mzee Yusufu #Chiku amefariki dunia usiku wakuamkia alipokuwa akijifungua na mtoto amefariki taarifa zaidi tutaendelea kupeana!!” – Geah Habib.
Chiku amekutwa na mauti  Jumamosi June 17,2017 jioni katika hospitali ya Amana, Ilala ya jijini Dar es Salaam alipopelekwa kujifungua.
Mzee Yussuf amesema alimpeleka mkewe Hospitalini hapo June 17,2017 saa 10 alasiri kwa ajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya alikutwa na mauti hayo baada ya upasuaji uliofanywa kutokwenda salama hivyo kusababisha kumpoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMINA
Tanzia: MKE WA MZEE YUSUF 'BI CHIKU' AMEFARIKI DUNIA Tanzia: MKE WA MZEE YUSUF 'BI CHIKU' AMEFARIKI DUNIA Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 4:30 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.