banner image

TAREHE KAMA YA LEO MIAKA MITANO (5) ILIYOPITA TANGU PATRICK MAFISANGO MUTESA ALIPOFARIKI

PATRICK MAFISANGO MUTESA
Leo imetimia miaka mitano tangu aliyekuwa mchezaji kiungo wa timu ya Simba,
 Patrick Mafisango Mutesa alipofariki dunia kwa ajali ya gari maeneo ya veta(chang'ombe road)

GARI ALILOPATA NALO AJALI MAFISANGO
 Mafisango aliyejiunga na Klabu ya Simba akitokea timu ya Azam Fc,  alizaliwa Machi 7, mwaka 1987, nchini Rwanda na kabla ya kutua nchini aliwahi kuichezea timu ya APR ya Rwanda. 
KIKOSI CHA SIMBA


Mchezaji huyo atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika Klabu ya Simba kwa kung'aa zaidi katika Ligi hiyo kwa kupachika mabao na kutoa pasi za mwisho, ambapo Mechi ya mwisho ya Mafisango ilikuwa ni kati ya Simba dhidi ya Al Ahly Shandy katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3. 
Mafisango aliweza kuifungia timu yake bao moja kati ya matatu.

MAFTAH  NA KAZIMOTO

BOBAN NA ISMAIL ADEN RAGE WAKITOA HESHIMA YA MWISHO SIKU YAKUMUAGA MAFISANGO

MAFTAH ALIEBEBA MSALABA AKIONGOZA WACHEZAJI WENZIE KUUBEBA MWILI WA MPENDWA WETU

JUMA NYOSO(KUSHOTO) +JOHN BOKO (KULIA) wakiwa wamebeba jeneza la MAFISANGO
Wana Simba, Wanamichezo na mashabiki wote kwa ujumla, tutakukumbuka siku zote mpendwa wetu Patrick Mafisango
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe Amina
TAREHE KAMA YA LEO MIAKA MITANO (5) ILIYOPITA TANGU PATRICK MAFISANGO MUTESA ALIPOFARIKI TAREHE KAMA YA LEO MIAKA MITANO (5) ILIYOPITA TANGU PATRICK MAFISANGO MUTESA ALIPOFARIKI Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 11:48 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.