SIR ANDY CHANDE |
Aliyekuwa Kiongozi wa jumuiya ya Freemason Tanzania na
Afrika Mashariki. Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande amekuwa mwanacham wa
Freemason kwa takribani miongo sita tangu ajiunge na umoja huo mwaka 1954.
Kiongozi huyo alizaliwa Mombasa Kenya Mei 7,1928 ingawa
wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini mkoani Tabora
Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa katika mitandao ya
kijamii juziAsubuhi. Kulingana na taarifa hizo kiongozi huyo alifariki dunia
jijini Nairobi alikokuwa akitibiwa. Kiongozi huyo anatarajiwa kuchwa jumanne
ijayo na kwamba wanataraji zaidi ya watu 300 kutoka nje na ndani ya nchi
watahudhuria mazishi yake.
HISTORIA YA SIR CHANDE
Sir Chande alizaliwa Mombasa Kenya Mei 7, 1928, ingawa
wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mkoani Tabora magharibi mwa Tanzania.
Alifika Tanzania
mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa
bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyaia kkazi.
Katika simulizi zake kadhaa, Sir Chande alisema alikutana na
watu wengi ambao walikuwa wanahudhuria vikao vya Freemason, akaanza kuuliza na
akajifunza mambo kadhaa kuhusu watu hao.
SIR ANDY CHANDE ENZI ZA UHAI WAKE AKIWA NA HAYATI BABA WA TAIFA |
Wakati huo, hao watu hawkuwa huru kuzungumzia Freemason kama
alivyokfanya Sir Chande, hasa kabla ya vita ya pili ya dunia.
Sir Chande alisema wakati huo Freemason ilikuwa imegawanywa
makundi tofauti, katika Hospitali, Shule, na mashirika mbalimbali na kulikuwa
na kundi maalum kwa ajili ya matajiri na wanafanyakazi wakubwa wa serikali.
Ukiangalia vizuri wengi wao walikuwa ni wazungu na Baadhi ya wahindi.
Kundi la kwanza lilikuwa linaongozwa na watu wa Scotland,
makundi mawili yliyofuata yalikuwa yanaongozwa na Waingereza na kundi la nne
lilikuwa linaongozwa na wahindi ambalo ndilo Chande alilojiunga nalo.
Ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na Freemason.
Aliapishwa rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wamiaka 28.
Kumbuka kwamba masharti ya kujiunga ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.
Baada ya hapo ndipo alipanda cheo nakupewa nafasi ya
kuongoza kundi au tawi la Freemason katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni
Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
Akajiunga na miradi tofauti ya Freemason nchini Uingereza
yakiwemo hoteli za kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hotel mpya ya
Freemason nchini Ghana kwenye mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari.
SIR ANDY CHANDE AKIWA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE TZ MHESHIMIWA DR.JK |
Hotel nyingine ya kifahari aliyoisimamia ujenzi wake iko
Zambia.
Sir Chande anakumbukwa sana kwa kuanzisha shule ya msingi ya
viziwi Buguruni, Dar es salaam, moja ya taasisi ambazo alizipa kipaumbele mno
hadi anaingia kaburini. Sir Andy Chande alistaafu kama kiongozi wa Freemason
Afrika mashariki mwaka 2005 baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, akawa hahudhuri mikutano ya
nchi hizi lakini akishiriki ile ya Uingereza kwa sababu alikuwa akiendele
kufanya kazi huko.
KWAHERI SIR ANDY CHANDE
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
10:14 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment