banner image

IMEPITA MIAKA 11 SASA, TANGU TULIPOMPOTEZA NGURI WA MUZIKI WA BENDI Shaban Ally Mhoja Kishiwa(a.k.a TX MOSHI)

TX Moshi Enzi za uhai wake akikung'uta gitaa

Kumbukumbu Kifo cha mpendwa wetu TX  Moshi tarehe kama ya leo miaka 11 iliyopita (29 March 2006)

Mpendwa wetu TX Moshi alifikwa na umauti tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya JUMATANO majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo makaburi ya Keko machungwa.

 Ndugu TX alijiunga Msondo mwaka 1982 akitokea Polisi Jazz. Miongoni mwa nyimbo alizotunga mara baada ya kujiunga ni pamoja na Ajuza, Asha Mwanaseif, (aliomtungia mkewe), na Ashibaye.

Alitunga nyimbo nyingi lakini nyimbo zilizotia fora sana ni pamoja na Kilio cha Mtu Mzima, Ndoa Ndoano, Piga Ua Talaka Utatoa, Ndoa ya Isihaka Kibene, Kaza Moyo na Ajali.

Wimbo wa Ajali aliutunga baada ya kupata ajali ya kuparamia mti wa mvinje pale Mivinjeni Desemba 16, 2005 iliyompelekea kuvunjika mguu.

Moshi alikua chakaramu na mbunifu wa kutunga vionjo ikiwemo mtindo ujulikanao kama Mambo Hadharani na katika nyimbo alipenda kuchombeza vionjo vyenye kutoa raha na kunogesha wimbo mfano utasikia "we nani", " kidogo tu..kidogo tu", "kwanini lakini", " watoto wanachezea umeme", "dispilin", " fair play" nk

Wakati wa uhai wake alipitia katika bendi mbalimbali za muziki ambazo ni pamoja na Safari Trippers, Juwata Jazz. UDA Jazz, na Polisi Jazz, ambayo alitokea wakati anajiunga msondo. Tz pis alijaliwa kupata tuzo mbalimbali mfululizo za muziki kama Kilimanjaro Music Award.


Ndugu Moshi alibatizwa jina la TX, na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi aliyekuwa mtangazaji wa Radio Tanzania, marehemu Julius Nyaisanga. Nyaisanga alimbatiza jina hilo kutokana na tunzi zake za uhakika. Nyaisanga alikua mtangazaji wa RTD na kisha vituo vya IPP Media. Jina halisi la TX ni Shaaban Mhoja Kishiwa ingawa alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la Moshi William TX.

Alizaliwa mwaka 1958 Korogwe Tanga.

Kwa kweli Tx Moshi ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa Msondo na ulimwengu wa muziki wa Dansi Tanzania. Tarehe 29 wana Msondo tumkumbuke na kumuombea dua daima baba yetu kipenzi.

Bofya Hapa Kutizama moja ya wimbo wa ottu jazz band 

 

 

IMEPITA MIAKA 11 SASA, TANGU TULIPOMPOTEZA NGURI WA MUZIKI WA BENDI Shaban Ally Mhoja Kishiwa(a.k.a TX MOSHI) IMEPITA MIAKA 11 SASA, TANGU TULIPOMPOTEZA NGURI WA MUZIKI WA BENDI  Shaban Ally Mhoja Kishiwa(a.k.a TX MOSHI) Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 12:22 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.