banner image

YALIYOJIRI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU AMINA ATHUMANI MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU NA MZALENDO KISIWANI ZANZIBAR.

R.I.P AMINA ATHUMAN      
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja leo. kutowa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.   
Kwa taarifa za msemaji wa familia Ndg Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu tasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao Lushoto siku ya Jumanne mchana. 

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya mazishi.
 Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu Ndg Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutowa pole leo asubuhi.
SOMA ZAIDI...
YALIYOJIRI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU AMINA ATHUMANI MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU NA MZALENDO KISIWANI ZANZIBAR. YALIYOJIRI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU AMINA ATHUMANI MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU NA MZALENDO KISIWANI ZANZIBAR. Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 5:22 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.