Waziri wa mazingira katika Serikali ya Burundi, Emmanuel Niyonkuru, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.
Polisi nchini wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kusema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.
Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi wameuawa tangu Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu 2015, hatua ambayo wapinzani wanasema ni kinyume na sheria.
Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.
Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.CHANZO:BBC SWAHILI
Waziri wa mazingira nchini Burundi auwawa kwa kupigwa risasi
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
3:51 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment