banner image

TAARIFA YA MAZISHI!

Tungependa kuwataarifu kwamba mwili wa ndugu yetu Leo Mapunda Mwakitalu umeweza kuondoka leo asubuhi, Jumatatu, Desemba 26, 2016 kwa safari ya kwenda Tanzania kwa mazishi kupitia Amsterdam, Uholanzi.

Kwa taratibu za mashirika ya ndege husika, mwili utalala Amsterdam, Uholanzi usiku wa Jumanne, Desemba 27, 2016 na hivyo kufika Dar Es Salaam, Tanzania siku ya Jumatano, Desemba 28, 2016 saa Tano Kasorobo usiku (10:45pm) kwa muda wa Tanzania.

Dada yetu Martha na watoto, alifanikiwa kuondoka jana Jumapili, Desemba 25, 2016 na wamefika Tanzania leo Jumatatu, Desemba 26, 2016. Mama mzazi wa marehemu, yeye alisafiri Jumatano, Desemba 21, 2016 na kufika Tanzania Alhamisi, Desemba 22, 2016.

Kwa Dar ES Salaam, Tanzania, msiba upo kwa wazazi wa marehemu, Sinza kwa Remy, Mtaa wa Muungano. Kwa maelezo zaidi ya kufika msibani, waweza wasiliana na ndugu wafuatao:

0758 808126 Leonard Mkude
0719 129024 Ena Mkude
0713 753113 Nkinde Mwakitalu
0713278562 Mboka Mwalugaja
0754281726 Isakwisa Kalinga

Kutakua na ibada siku ya Alhamisi, Desemba 29, 2016 kuanzia saa 8 mchana (2pm) katika kanisa la Kilutheri - Magomeni mviringo. Mazishi yamepangwa kufanyika katika makaburi ya Kinondoni kuanzia saa 10 jioni (4pm) siku ya Alhamisi, Desemba 29, 2016.

Kwa Mara nyingine tena, tunawashukuru wote waliohusika kwa maombi, mali, na hali katika kulifanikisha suala zima la kuweza kumsafirisha mpendwa wetu Leo Mapunda Mwakitalu kwa mazishi, na pia kuwawezesha Martha, watoto, na Mama mzazi wa marehemu kusafiri pia.

Tunaomba tuendelee kuiweka katika maombi familiya ya ndugu yetu mpendwa Leo Mapunda Mwakitalu.

Tunatanguliza shukurani,
Kamati ya Maandalizi


Source:http://lukemusicfactory.blogspot.com/
TAARIFA YA MAZISHI! TAARIFA YA MAZISHI! Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 3:54 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.