banner image

MIILI YA WATAFITI WALIOUWAWA NA WANANCHI YAAGWA JIJINI ARUSHA


Baada  ya baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi katika  Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuwaua watafiti wa Kituo cha Udongo na Maendeleo cha Selian Arusha, wakazi wa kijiji hicho wamehama makazi yao wakihofia kukamatwa na Jeshi la Polisi.

Waandishi wa habari waliofika kijijini hapo jana na walishuhudia hali ya utulivu kijijini hapo tofauti na ilivyozoeleka.

Pamoja na wananchi hao kukimbia makazi yao, taarifa zinasema viongozi wote wa Serikali ya Kijiji hicho  wamekamatwa na polisi wakiwamo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Albert Chimanga na Diwani wa Kata ya Iringa Mvumi, Robert Chikole.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Michael Kagisi, alisema kitendo cha wananchi kukimbia kijiji hicho kimesababisha shughuli nyingi za  jamii kusimama   na maduka kufungwa


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 


Source: http://lukemusicfactory.blogspot.com/2016/10/miili-ya-watafiti-walioua-na-wananchi.html#more 


CONVIDA Inawapa pole Ndugu na jamaa Wa Marehemu, kwa kuondokewa nawapendwa wao, Bwana ametoa na Bwana ametwa jina Bwana liImidiwe.
Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahala pema na peponi. Amen
MIILI YA WATAFITI WALIOUWAWA NA WANANCHI YAAGWA JIJINI ARUSHA MIILI YA WATAFITI WALIOUWAWA NA WANANCHI YAAGWA JIJINI ARUSHA Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 2:14 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.