Mwaka 1995, Dk. Masaburi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar e Salaam .
Mbali na hilo pia alibahatika kuwa na Shahada ya Juu ya Masuala ya Ugavi
iliyotolewa na Bodi ya Uhasibu ya Taifa (NBAA), huku kwa miaka kadhaa
akifanikiwa kuwa mfanyakazi wa Kiwanda cha vinywaji cha Chibuku.
Pia amefanyakazi Wizara ya Elimu, Utamaduni na Michezo kupitia mradi
maalumu wa Benki ya Dunia (WB) na amekuwa akimiliki Shule ya Sekondari
ya Dk. Didas Masaburi iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam pamoja na
anamiliki Chuo cha Ugavi na Manunuzi kilichopo Chanika.
Dk. Masaburi alikuwa akiishi na figo moja kwa tangu mwanzoni mwa miaka 2000 hadi mauti yanamkuta.
Safari ya siasa
Mwaka 2015, marehemu Dk. Didas Masaburi, alijitosa katika kunyang’anyiro
cha ubunge katika jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ambapo alishindwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Saed Kubenea ambaye
alitangazwa kuwa mbunge hilo kwa kura 87,666 huku Masaburi akipata kura
59,514.
Mwaka 2010, Dk. Masaburi alichanguliwa kuwa Diwaniwa wa Kata ya Kivukoni
na Desemba 23, akachaguliwa kwa Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa
kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha uchaguzi uliofanyika kwenye
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo aliwashinda wapinzani
wake, Diwani wa Kata ya Tandale, Amir Mbunju (CUF).
Meya huyo wa zamani alichaguliwa kwa kura 125 huku wajumbe wanne kati yao hawakupiga kura na 9 ziliharibika.
Kauli tata za kukumbukwa
Agosti 6, mwaka 2011, Dk. Masaburi aliingia katika malumbano ya wabunge
wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao walimtaka ajiuzulu kutokana na kukiuka
taratibu katika uuzwaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).
Kutokana na hali hiyo meya huyo wa zamani alijibu mapigo dhidi ya
wabunge hao ambapo alisema baadhi yao wanashindwa kufikiri kwa kutumia
vichwa na badala yake wanafikiri kwa kutumia ‘makalio’.
Alisema wabunge katika kuchangia hoja ya suala la UDA wamegawanyika
katika mafungu matatu ambao alisema katika mafungu hayo moja halijui
lolote kuhusiana na sakata hilo na limedandia tu hoja.
Alitaja kundi la pili kuwa ni la wabunge wa jiji la Dar es Salaam ambao
ni Mbunge wa Ubungo wa wakati huo, John Mnyika, na Mbunge wa Kawe,
Halima Mdee, ambao alisema wanatafuta umaarufu wa kisiasa kupitia sakata
la UDA.
Alisema Mnyika aliweza kuhoji hata katika vikao rasmi, lakini Mdee hajui chochote kwa kuwa hajawahi kuhudhuria vikao vya jiji mpaka sasa.
Alisema Mnyika aliweza kuhoji hata katika vikao rasmi, lakini Mdee hajui chochote kwa kuwa hajawahi kuhudhuria vikao vya jiji mpaka sasa.
Aidha, kundi la tatu ambalo ndilo alilituhumu zaidi kufikiri kwa kutumia
“makalio” badala ya kichwa ni la wabunge Abasi Mtemvu aliyekuwa
(Temeke), Mussa Azzan ‘Zungu'(Ilala) na Dk. Makongoro Mahanga aliyekuwa
(Segerea) ambao alidai kuwa wanajua ukweli wa jambo hilo lakini
wanapotosha ili kuficha madhambi yao ambayo alisema yataibuliwa muda si
mrefu ya ufisadi ndani ya jiji hilo.
Escrow yamuibua
Kutokana na sakata hilo ambalo liliitikisa Serikali ya awamu ya nne
chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Dk. Masaburi alijitokeza hadhani
baada ya makombora kutoka kwa wabunge na kutaka kiongozi huyo wa nchi
kutobebeshwa mzigo huo.
Alisema Rais Kikwete amefanyakazi kubwa ya kuhakikisha anawashughulikia waliohusika hivyo hastahili kuingizwa kwenye kapu hilo.
Tukio la mwisho
Kabla ya kufikiwa na mauti Dk. Masaburi alipelekwa nchini India mara
mbili kwa ajili ya matibabu na kwa mara ya mwisho alionekana hadharani
Serena Hoteli ambapo alikwenda kutoa mada kuhusu masuala ya manunuzi.
Baada ya kutoa mada akiwa njiani anarejea nyumbani kwake alijisikia vibaya na shinikizo la damu kushuka ambapo alikwenda hospitali kwa matibabu.
Baada ya kutoa mada akiwa njiani anarejea nyumbani kwake alijisikia vibaya na shinikizo la damu kushuka ambapo alikwenda hospitali kwa matibabu.
Source:http://lukemusicfactory.blogspot.com/2016/10/historia-fupi-ya-marehemu-didas-masaburi.html#more
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU DK. DIDAS MASABURI
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
4:52 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment