banner image

HUYU NDIO SIR GEORGE KAHAMA (One year Death anniversary of Sir George Kahama)

Balozi Clement George Kahama

WASIFU WA BALOZI SIR CLEMENT GEORGE KAHAMA
Balozi Clement George Kahama, aliyejulikana zaidi kama Sir George alizaliwa tarehe 30 Novemba, 1929 katika Wilaya ya Karagwe na kufariki dunia tarehe12 Marchi, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa Figo Renal Failure)  kwa takribani miaka miwili.
Katika uhai wake, Sir George alifanyakazi katika Serikali kwa vipindi mbalimbali zaidi ya miaka 50 ikiwemo awamu tatu za uongozi wa taifa hili baada ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961. Marehemu Sir George alikuwa miongoni mwa waafrika wachache waliopata fursa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria yaani  Legislative Council mwaka 1957 na miaka miwili baadaye kuteuliwa kuwa Waziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito ya kikoloni kuelekea uhuru kwa nafasi ya Waziri wa Ushirika na Ustawi wa Maendeleo ya Jamii akiwa na Wenzake wazalendo Chief Abdalah Fundikira, Amir Jamal, na Solomon Eliufoo na Mwalimu akawa Waziri Kiongozi ( Chief Minister).
Baada ya Uhuru Mwaka 1961, Mhe Balozi George Kahama aliteuliwa kuwa Waziri wa kwanza wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Baraza la Mawaziri la Watu tisa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru.Kutoka Uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 2005 Sir George Kahama aliuteuliwa na Baba wa taifa na baadaye Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, kushika nyazifa za Wizara mbalimbali serikalini zikiwemo Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, Wizara ya Biashara na Viwanda, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ushirika na Masoko, Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma na wakati huo  huo akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).
Katika muda wote wa utumishi wa Umma, Sir George aliaminiwa sana na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere baadaye Mhe Benjamin Mkapa kwa nyakati tofauti waliweza kumtuma katika nchi mbalimbali kuwa wakilisha kama mwakilishi maalum wa Rais (Special Envoy) katika nchi mbalimbali ikiwemo Zaire ambayo sasa  inajulikana kama DRC, Burundi na Rwanda,  Holy See (Vatican) na nchi nyingine.
Kazi nyingine alizowahi kufanya Mhe Sir George Kahama ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Maendeleo la taifa (NDC),taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia uanzishwaji wa Viwanda nchini, Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa Kituo  cha Kuvutia wawekezaji (IPC) ambacho baadaye kimekuja kujulikana kama  Tanzania Investment Centre-TIC. Kablaya Uhuru Sir George alikuwa kiongozi wa Chama cha ushirika cha Bukoba, chama ambacho kilitoa msaada mkubwa wa hali na mali katika kusaidia harakati za ukombozi na kuimarisha TANU kama ilivyokuwa kwa vyama vingine vya Ushirika katika maenembalimbal nchini. Itakumbukwa kuwa Wazalendo watano waliounda Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito mwaka 1959 akiwemo Mzee Paul Bomani, Chief Abdullah Fundikira (Tabora), Solmon Eliufoo (Kilimanjaro), Amir Jamal ( Morogoro) na Kahama Mwenyewe (Kagera) walikuwa viongozi katika vyama vya ushirika katika maeneo waliyotoka.
Aidha, katikaUhai wake, Sir George Kahama aliwahi kutumikia taifa katika  nyanja za kidiplomasia kama Balozi wa Tanzania Ujerumani mwaka 1965-1966, Baloziwa Tanzania China (1984- 1989) na Balozi wa Tanzania Zimbabwe (1989-1991).
 Katika uhai wake, Sir George aliwahi kutunukiwa nishani mbalimbali zakitaifa na Kimataifa ikiwemo Knight Commander of the Order of St. Gregory the Great iliyotolewana Pope John XXIIImwaka 1962. 
Hii ndiyo nishani iliyozaa jina la Sir George
Nishani zingine ni kama“The Order of Kilimanjaro iliyotolewa na RaisMstaafu Ali Hassan Mwinyi 1990,ambayo ni nishani yajuu kabisa wanayo tunukiwa watumishi wa umma. Mwaka 1975-1976 alikuwa Mjumbe wa Kundi la Watu Mashuhuri duniani walio teuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya utafiti kuhusu athari za Uendeshaji wa Makampuni Makubwa ya Kimataifa katika uchumi wa nchi zinazo endelea.
Mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Chama cha Mapinduzi na Serikali ikiwemo Serikali kuhamia Dodoma kwa kasi kubwa na chama kuimarika zaidi kumetokea siku chache kabla ya kufariki kwake na kutimiza ndoto yake zaidi ya miaka 40 aliyo jishughulisha na mradi wa Ustawishaji wa Makao Makuu.
Mwaka1976, Sir George aliteuliwa na Serikali ya Nigeria kama Mjumbe wa Kamati ya watu watatu waliopewa kazi ya kufanya tathmini ya mchakato wa uhamishaji wa Mji Mkuu wa Nigeria kutoka Lagos kwenda Abuja.
JK akiwa katika picha ya pamoja na Joseph Kahama(Wanne kushoto) ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu maisha ya mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama. wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu hicho,uliofanyika jijini Dar(March 27,2010). Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, Sir George Kahama(wapili kushoto) na kulia ni Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi.

Sir George aliwahi kuandika maandiko na vitabu mbalimbali katika Nyanja za Kidiplomasia,  Ushirika, Uchumi,  Maendeleo ya Ujenzi,ikiwemo kitabu cha “The Challenge for Tanzania’s Economy” kilicho chapishwa na kampuni ya JamesCurrey Heinemann ya Uingeleza na “Tanzania into the 21stCentury”,pia alichangia kuandika kitabu cha “The First Tanganyika Industrial Development Blue Print” pamojana  Arthur D. Little Inc. ya Marekani.
Mbali na utumishi Serikalini, Sir George Kahama alikuwa Baba mzuri wa familia aliyependa umoja wa familia na alikuwa baba tuliyemtegemea kwa ushauri na dira katika maisha yetu.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe
HUYU NDIO SIR GEORGE KAHAMA (One year Death anniversary of Sir George Kahama) HUYU  NDIO SIR GEORGE KAHAMA (One year Death anniversary of Sir George Kahama) Reviewed by SHEDrack Mtawa on 2:53 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.