![]() |
KAPTEN JOHN KOMBA |
NA HII NDIO HISTORIA FUPI YA MAREHEMU KAPTEN JOHN KOMBA.
Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945, alipata elimu ya msingi katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1975 hadi mwaka 1976, John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Mkoani Iringa,ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
John Komba Alikuwa ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.
Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
MIAKA MITATU (3) YA KUMBUKIZI YA KIFO CHA CAPTAIN JOHN KOMBA
Reviewed by SHEDrack Mtawa
on
11:00 AM
Rating:

No comments:
Post a Comment