Askofu Castory Msemwa enzi za uhai wake |
Na Bernard James, Dar es salaam
JIMBO Katoliki Tunduru Masasi
limempoteza Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Castory Msemwa aliyefariki
dunia leo majira ya saa 7 mchana nchini Oman.
Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo
Katoliki Tunduru Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki
dunia akiwa mjini Muscat (Oman), akiwa safarini kwenda nchini India
kupata matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
“Amefariki nchini Oman wakati akienda
kupata matibabu nchini India. Akiwa nchini humo amezidiwa ghafla na
kupoteza fahamu, hadi umauti ulipomkuta.”
Marehemu Msemwa amekuwa na tatizo la
kiafya kwa kipindi cha miaka miwili, na amekuwa akipata tiba mbalimbali
na kuendelea na utume kama kawaida.
Aliondoka nchini siku ya Jumatano wiki hii kuelekea nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.
Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu
wa kuuleta nchini mwili wa marehemu Askofu Castory Msemwa siku ya
Jumapili Dar es Salaam unafanyika. Taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi
zitatolewa baadaye.
Askofu Castory Paul Msemwa amezaliwa mwaka 1955 katika kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya
Motola, kisha Sekondari katika Seminari Kuu ya Peramiho ambapo alisomea
Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987.
Alipata daraja ya Upadri tarehe 7 Juni
1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, Kiongozi wa vijana parokiani jimboni
Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum Pontifical College
for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996.
Alipata Daraja ya Uaskofu tarehe 30 Januari 2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi tarehe 25 Agosti 2005.
Alipata Daraja ya Uaskofu tarehe 30 Januari 2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi tarehe 25 Agosti 2005.
Mwenyezi Mungu ampumzishe pema mbinguni, Amina.
Tanzia : ASKOFU WA JIMBO LA TUNDURU MASASI CASTORY MSEMWA AMEFARIKI DUNIA
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
9:45 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment