banner image

Miaka miwili (2) yakumbukumbu ya kifo cha Christopher Mtikila

Mtikila alizaliwa Njombe, kusini mwa Tanzania, mwaka 1950.

Historia yake
Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) ambacho kina
usajili wa kudumu hapa Tanzania.
Pamoja na shughuli za siasa, Mchungaji Mtikila ni mwanzilishi na mkuu wa Kanisa la Kipentekoste la Full Salvation. Lakini pia kwa muda mkubwa wa maisha yake amekuwa anajihusisha na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho “Liberty Desk”. Kanisa lake ni moja ya makanisa machache hapa Tanzania yenye vitengo vya namna hiyo.
Umaarufu wa Mtikila ulikua sana mwanzoni mwa miaka ya 1990 kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuongea, upinzani wake dhidi ya muundo wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, madai yake kuhusu kile anachokiita “uhujumu wa uchumi unaofanywa na watu ambao anawaita magabacholi” na kesi mbalimbali za kikatiba alizokuwa akifungua katika Mahakama za Tanzania, ni kati ya mambo machache yaliyomfanya asikike kila kona ya nchi.

Kwa muda mrefu, chama chake cha DP hakikuweza kupata usajili wa kudumu kutokana na kukataa kwake kuitambua Zanzibar. Alikuwa akisisitiza kuwa chama chake ni cha Tanganyika na siyo Tanzania. Hata hivyo, ilimpasa abadili msimamo wake katika miaka ya hivi karibuni kwa kukubali kutafuta wanachama kutoka Zanzibar (kama sheria ya uchaguzi inavyotaka) ndipo kikapata usajili wa kudumu.
Mtikila alifungwa kwa mwaka mmoja mwaka 1999 baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba. Mwaka 2004 pia alihukumiwa kifungo kilichosimamishwa cha miezi sita kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya mkuu wa polisi wa wilaya ya Ilala. Kwa ujumla maisha yake yamekuwa ni ya harakati muda wote, akipambana awezavyo, akisimama kidete inavyowekana na akijikuta matatani kila uchwao.
Mchungaji Mtikila amemuoa Georgia na wana watoto.
Miaka miwili (2) yakumbukumbu ya kifo cha Christopher Mtikila Miaka miwili (2) yakumbukumbu ya kifo cha Christopher Mtikila Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 3:56 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.