Julius Kambarage Nyerere was a Tanzanian anti-colonial activist, politician, and political theorist.
Born: April 13, 1922, Butiama, Tanzania
Died: October 14, 1999, London, United Kingdom
Misemo ya Hekima ya Mwl. J. K. Nyerere
“inawezekana, timiza wajibu wako” Mwl JK Nyerere.
“Ikulu ni mahali patakatifu, anaye kimbilia ikulu niwa kuogopwa kama ukoma” Mwl JK Nyerere.
“Ccm sio mama yangu” Mwl JK Nyerere.
“Niliamua waziri achapwe viboko kwa rushwa akitoka amsimlie mkewe”. Mwl JK Nyerere.
“Mtanzania wa leo hawezi kununua watu kabla ya yeye hajanunuliwa!!!”. Mwl JK Nyerere.
“Habari ni habari utasikia fulani kampiga mkewe hiyo si habari, lakini Nyerere kampiga mkewe hiyo ni habari itaandikwa kwelikweli”. Mwl JK Nyerere.
“Kiongozi atakayepokea rushwa, tukimkamata tutamfunga miaka miwili na atapigwa viboko 24; 12 akiingia na kumi nambili akitoka, aende akamwonyeshe mkewe. Mwl JK Nyerere.
“Katika nchi kama yetu, ambayo Waafrika ni maskini na wageni ni matajiri, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi, katika miaka themanini au miaka ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni, na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.” [NYERERE, 1958]
“Watanzania wanataka mabadiliko; wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM”
Julius Nyerere, Dodoma, 1995. . Mwl JK Nyerere.
“Nang’atuka, lakini bado nasisitiza kuwa, bila CCM imara nchi yetu itayumba” 1990s. . Mwl JK Nyerere.
“Serikali ikitawaliwa na rushwa haiwezi kukusanya kodi, itabakia kukimbizana na watu wadogo wadogo tu”. Mwl JK Nyerere.
“Serikali ya Tanzania haina Dini”. Mwl JK Nyerere.
“Zambi ya ubaguzi itawarudi tu naomba Mungu anisamehe lakini na iwarudi”. Mwl JK Nyerere.
“Mimi nang’atuka, lakini naendelea kuamini bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba”. Mwl JK Nyerere.
“CCM si mama yangu, ikiacha misingi yake nami naicha” J.K Nyerere
“Mimi nimekaa Ikulu miaka 21, kuna biashara gani pale Ikulu?. Mwl JK Nyerere.
” Mara hii tu mmetajirika kiasi hicho? Kama mmeweza kutajirika kiasi hicho katika muda mfupi, fanyeni basi wote tutajirike, kwa nini mtajirike peke yenu?!”. Mwl JK Nyerere.
“Kwa mtu mwaminifu kabisa, Ikulu ni mzigo, si mahali pa kukimbilia hata kidogo”. Mwl JK Nyerere.
KUMBUKIZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE ALIYEFARIKI TAREHE KAMA YA LEO MIAKA 18 ILIYOPITA
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
12:45 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment