Familia
ya Alhaj Sudi Suleiman Madega, Katibu Mkuu (Mst) Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).
Inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa
ndugu, jamaa na marafiki kwa msaada wa hali, mali na faraja walioipatia familia
katika kipindi kigumu cha kuuguza, msiba na hatimaye kumpuzisha kwenye nyumba
yake ya milele mpendwa wao Hajat Mwalimu Batoul Abdallah Mbarouk aliyefariki
tarehe 16 Agosti, 2017 na kuzikwa tarehe 17 Agosti, 2017.
Hajat Batoul A.
Mbarouk alikuwa Mke wa Sudi S. Madega; na Mama wa Suleiman, Amir, Dr. issa,
Maryam, Zuhura na Asha Madega. Pia, Mkwe wa Maryam Hamza Chum, Nuru Kassim Kisesa,
Daud Buswelo na Hawa Kadyanji.
Kwa
kuwa ni ngumu kumshukuru kila mmoja, itoshe kusema ahsanteni sana nyote. Hata
hivyo, kipekee familia inapenda kufikisha salamu maalum kwa wafuatao:-
i.
Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Taasisi
ya Saratani Ya Ocean Road ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwaka huu
mwanzoni na hatimaye kuaga dunia tarehe 16 Agosti, 2017. Hususa, Dr. Steve, Dr.
Kezia , Dr. Mathew, Dr. Chacha, Dr. Ruta
Dr. Abdi Sangali , Sister Sapine,
Sister Wema , Sister Ester , Sister Doris , Sister Kimath , Sister Eliza
, Joel Makanyaga, Mkulia, Alawi, Solomon na wengine wote;
ii.
Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwezi
Agosti, 2016;
iii.
Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais (Mst) wa
Jamhuri Muungano wa Tanzania na mkewe Mh. Mwl. Salma Rashid Kikwete (Mb) na
familia yao;
iv.
Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU);
v.
Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama
cha Walimu Tanzania (CWT). Hususan, Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa
Pwani na Walimu wote;
vi.
Mh. Jaji (Mst) Harold R. Nsekela (Kamishna wa
Maadili), Uongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma;
vii.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg. Kailima Ramadhani
na Mkurugenzi wa Utawala Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Hamis A. Mkunga;
viii.
Alhaji Masoud Msangi, Mkurugenzi Mtendaji
Nduvini Auto Works;
ix.
Majirani wa marehemu wa Mbagala, Mbezi na
Chang’ombe;
x.
Vile vile, tunapenda kutambua familia
zifuatazo:-
Ukoo wa Kanyama na Mbarouk
popote pale walipo, Familia ya Mh. Luteni (Mst) Abdallah Kihato, familia ya Mh.
Mohamed S. Jegame, familia ya Marehemu Balozi Isaya Bakari Chialo, familia ya Dr.
Hamza Juma Chum, familia ya Brigedia Jenerali (Mst) Ussi Khamis wa Zanzibar, familia
ya Kassim Kisesa, familia ya Masoud Sultan, familia ya Bakari O. Sangali, familia
ya Issa Sechonge, familia ya Kisarazo, familia ya Idris Mavura, familia ya
Marehemu Mwl. Hemed Ally Kimeah, familia ya Mbaruku Nguzo, familia ya Mbegu na
wengine wote.
Pamoja na salamu
hizi, familia inawaarifu na kuwaalika
rasmi katika Arobaini ya Marehemu Mwalimu Mbarouk itakayofanyika nyumbani
kwake Mbagala siku ya jumapili tarehe 24
Septemba, 2017 kuanzia saa 5 asubuhi mpaka 8 mchana.
Kwa mawasiliano tafadhali
wasiliana na Ndg. Amir Sudi Madega kupitia Namba 0716875737.
Innalilahi
Wainailahi Rajioun,
Ahsanteni
Sana
SALAMU ZA SHUKRANI NA MWALIKO WA HITMA YA MAREHEMU HAJAT MWL. BATOUL ABDALLAH MBAROUK
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
1:55 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment