banner image

KWAHERI SIR GEORGE KAHAMA


Mmoja wa waasisi wa uhuru na  aliyewahi kiwa mtendaji mkuu wa serikali ya tanganyika SIr George Kahama ( 88) alifariki dunia Dar es salaam jana.
Kahama maarufu kama Sir George kahama alizaliwa Novemba 30, 1929. Na aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani (1961-1962) kabla 
    nafasi hiyo haijachukuliwa na Oscar Kambona kwa mwaka mmoja kuanzia 1962 hadi 1963.
      Sir Kahama alikuwa mtumishi wa wa Umma kwa miaka mingi na mwanasiasa mahiri na makini,katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika za kudai uhuru katika miaka ya 1950 hadi kujitawala mwaka 1961.
           Mwanasiasa huyo alipelekwa Uingereza na Chama cha usharika wa kahawa cha jimbo lililokuwa likiitwa Ziwa Magharibi  wakati huo,likiwa la wilaya za bukoba, Karagwe, Bihara mulo na Ngara.(kwasasa ni mkoa wa Kagera).
      Mwalimu Nyerere alifurahi akawa na matumaini ya kusaidiwa, kwanza kwasababu  alikwisha kuona ushirikiano wa Watanganyika  wengine hivyo akajua hata Kahama atamsaidi.
    Kwamujibu wa Sir George, katika mahojiano yake kabla ya kupatwa na mauti, alisema tumaini la mwalimu Nyerere wakati huo lilizidishwa na ukweli kwamba wao ni watani wa jadi.
       Sir George aliingizwa kimyakimya katika harakati za kudai uhuru wa iliyokuwa Tanganyika
     Alikuwa rafiki mkubwa wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, chanzi cha Urafiki wai likiwa ni jibu la jinsi gani alivyoingizwa kwa siri  katika siasa za katika siasa za Tanganyika.
        Wakati inaundwa Seriali baada ya Uhuru ndipo Mwalimu Nyerere alipomwita Sir George kutoka Bukoba ajiunge na  Baraza la Mawziri la serikali hiyo na akamteua kuwa Wazirinwa Ushirirka  na masako  na mwenyewe (Nyerere) akawa waziri mkuu.
        Baaadhi ya mawaziri walioteuliwa  walikuwa Paul Bomani, Chief  Abdallah Fundikira, Rashid Mfaume Kawawa, Solomon Eliofo, Nsilo Swai, Said Maswanya, Dereck Noel Bryceson, Sir Ernest Versey,  na Amiri Jamal.
     Sir George alikuwa Waziri wa kwanza wa mambo ya Ndani ya Nchi na baadaea Rais mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin mkapa alimteua tena kwa Waziri wa ushirika.
Kwahakika Hatutamsahau.
Mungu ailaze Roho ya mpendwa wetu Sir George mahala pema peponi. Amen
KWAHERI SIR GEORGE KAHAMA KWAHERI SIR GEORGE KAHAMA Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 12:25 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.