Mpendwa Mama Elise Job Kisyombe |
BORN: 1 Mei 1934
DIED: 18 January 2017
Dr Victooria na wambolezaj wengine wakiingia kanisani kwenye ibada ya mpendwa mama yetu |
Ndugu na jamaa wakitoa heshima ya Mwisho |
HISTORIA FUPI YA MPENDWA MAMA YETU; ELISE JOB KISYOMBE
Mpendwa Mama Elise J. Kisyombe alizaliwa Tarehe 1 Mei 1934 huko Kyela mkoani Mbeya. Alikuwa binti wa sita(6) wa Mzee Alick Mwakibete.
Ilikuwa ni mwaka 1953 mama yetu mpendwa na mpendwa baba yetu, Bw. Job Robinson Kisyombe, kwa ndoa takatifu ya kikristo katika kanisa la Morovian, Tukuyu. kuanzia mwaka 1953 waliishi maisha ya amani na furaha huko Tukuyu,Kyela,Iringa,Morogoro na Ifakara.
Baadae Baba alipata wadhifa wa kuwa Afisa Ujamaa na Ushirika wa Mkoa, Mama akiwa ni mama wa nyumbani alikuwa ni msaada mkubwa kwa Baba na alionyesha ushujaa na upendo kwa familia yake, na Taifa kwa kuzunguka mikoa mingi, kwa pamoja wakilitumikia taifa. Walifanya kazi mikoa ifuatayo: Singida, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, na mara tatu waliishi Iringa na mwisho walimalizia mkoa wa Mbeya hadi mwaka 1980 ambapo Baba alistaafu.
Mwaka 1975 walimpoteza binti yao wapili kuzaliwa Joyce Kisyombe alifariki katika Hospitali ya KCMC Moshi. Pili kwa masikitiko makubwa BABA yetu mpendwa Mzee Job Robinson Kisyombe aliitwa na Bwana tarehe 30 November 2008 na kuzikwa Mbeya. Misiba hii ilikuwa pigo kubwa kwa Mama Elise lakini wakati wote aliendelea kuishi maisha ya kumtumaini Mungu.
Mnamo mwaka 2007 mama yetu aligundulika na tatizo la kisukari. Hali hiyo ilibadilika ghafra mwaka 2012, familia ilimpeleka hospital ya Apollo, Hyderabald, India, amako madaktari walilazimika kukata mguu wake wa kulia. Pamoja na shida hii kubwa Mama Elisa alikuwa ni mtu wa furaha na shukrani wakati wote na aliendelea kuishi maisha ya kumtegemea Mungu.
Sisi sote tunamkumbuka Bibi Elise, kwa upendo wake mwingi kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo. wote tulio mfahamu tumebaki na kumbukumbu ya uso wenye kicheko na furaha, hali iliyomfurahisha kila aliyekutana naye. Alikuwa mkarimu, mpole na mwenye kupenda kujali ndugu. Bibi alikuwa kipenzi cha watoto na wajukuu wote nayeye alionyesha mapenzi makubwa kwa watoto na wajukuu wote wa ukoo wa Kisyombe,Mulenga, Nyondo, Kipuyo, Rukeha na wengineo.
Bibi na Babu walikuwa waumini wa sharika mbalimbali za KKKT katika miji yote waliyozunguka nchini. Nyumbani Mbeya waliabudu katika kanisa la Morovian, Usharika wa Ruanda. mpaka mauti yanamkuta alikuwa msharika wa kijitonyama Lutheran mwenye namba 1204 na pia mwana jumuiya wa sayuni. Kwa hesima ya bibi Jumuiya ya sayuni iliweka kambi la kudumu nyumbani kwa binti yake Dr. Victoria, ili kumwezesha bibi kushiriki Ibada pamoja nao. Siku zote akiulizwa aseme neno lolote, Bibi hujibu "nawashukuru sana" akiambiwa chagua wimbo alikuwa akichagua "Yesu Unipendaye, kwako nakimbilia". Alitambua kimbilio lake ni kwa Bwana Yesu.
Mungu alimpa kibali chakushiriki Ibada ya mwisho Usharikani Kijitonyama Jumapili ya tar. 8-January-2017. Siku hiyo alipokea baraka na kupiga picha na Baba Askofu. Hii ilikuwa picha yake ya mwisho hapa Duniani.
Mpendwa Bibi Elise, alitibiwa katika Hospital mbalimbali hapa nchini zikiwemo Hospital ya Rufaa Mbeya, Rufaa Muhimbili, Hindu Mandal, Eden Clinic, CCBRT na pia Hospital ya Apollo, Hyderabad, India ambako alikwenda mara mbili.
Ilikuwa ni siku ya jumatano, tarehe 18 January 2017, ambapo baada ya kuamka na kunywa chai Mpendwa alichukua Biblia yake na kusoma neno la Mungu akitumia kalenda ya KKKT. Hii ilikuwa ratiba yake kila siku asubuhi. baada ya kusoma na kutafakari Neno la Mungu Mpendwa bibi alijilaza kupumzika na ndipo aliitwa na Bwana. Bibi alipata neema ya Kuondoka katika maisha haya kwa Amani kama mtoto mchanga.
WATOTO WA MPENDWA BI. ELISE JOB KISYOMBE
Dr. Victoria Kisyombe,
Joyce Kisyombe(amesha lala)
Hilda Kisyombe
WAJUKUU WA MPENDWA BIBI ELISE
Janet,
Daniel,
Dr. Nai
Doreen.
KITUKUU WA BIBI ELISE JOB KISYOMBE
Moses
CONVIDA INATOA POLE KWA NDUGU NA JAMAA KWA KUMPOTEZA MPENDWA WETU BIBI ELISE JOB KISYOMBE, BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA; JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN
IN LOVING MEMORY OF MAMA ELISE JOB KISYOMBE
Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED
on
6:04 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment