banner image

WAZIRI MKUU AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA WALIOFARIKI KWA TETEMEKO BUKOBA

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole  wafiwa  wakati alipokwenda mjini Bukoba Septemba 11, 2016 kukagua athari za tetemeko la ardhi na kuwafariji majeruhi, wafiwa na wananchi wa mkoa wa Kagera. Alikuwa katika Ibada ya kuwambea marehemu hao kwenye uwanja wa Kaitaba .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu walipoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi  mkoani kagera katika ibad maalum ya kuwaombea marehemu hao iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)









WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea (siku Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.

 

Source: http://fullshangweblog.com/home/2016/09/11/waziri-mkuu-aongoza-wananchi-kuaga-miili-ya-waliokufa-kwa-tetemeko-bukoba/



Convida Funeral Home Company ltd Inatoa pole kwa Familia zote za wafiwa na wahanga wa tetemeko la Ardhi lilotokea Bukoba Siku ya jumamosi (10/09/2016).  Mungu azipumzishe Roho za Ndugu zetu Mahali pema peponi

Amen

WAZIRI MKUU AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA WALIOFARIKI KWA TETEMEKO BUKOBA WAZIRI MKUU AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA WALIOFARIKI KWA TETEMEKO BUKOBA Reviewed by CONVIDA FUNERAL HOME COMPANY LIMITED on 5:10 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.